Wednesday, May 21, 2014

JINSI YA KUTUNZA NGOZI YAKO.

Habari mpendwa,
 Leo tutazungumizia swala  la kutunza ngozi yako (skin care routine).
Awali ya yote kabla sijasema mengi ni vvema utambue kuwa unahitaji kuijua ngozi yako kabla ya kufahamu namna ya kuitunza! Je, unaijua ngozi yako?
Aina za ngozi.
Duniani kuna aina kuu tano za ngozi;
1.Ngozi ya mafuta.(Oil skin).
Sifa zake.
-Huwa inang'aa sana,
-Huwa haizeeki haraka,
-Huwa inatabia ya kutoa chunusi,
-Huwa haipati mikunjo haraka,
-Mwenye ngozi ya mafuta akipaka Make up zinapotea ndani ya muda mfupi.
2.Ngozi kavu.(Dry skin).
Sifa zake
-Huwa inapasuka pasuka,
-Ni rahisi sana kuzeeka na hupata makunyanzi  mapemaaa.
-Huwa inapauka  sana ukipaka Make up zinakaa muda mrefu.

3.Ngozi ya changanyiko(combination skin) 
 Ngozi hii inakuwa  na tabaka upanda mafuta upande kavu au kinyume chake.
Sifa zake.
 -Utakuta mashavuni pana mafuta  na paji la uso hakuna au kinyume chake.

4.Ngozi ya kawaida (Normal skin).
-Huwa haina tatizo lolote,
-Huwa haipati shida wala reaction yoyote
-Chochote utakachotumia twende tu.

5.Ngozi korofi (sensitive skin)
Sifa yake kuu ni kwamba chochote utakachotumia kinaleta shida, (reaction). Ngozi hii inachagua sana  (selective).Sabuni au Mafuta  kwa aina hii ya ngozi lazima yachaguliwe kwa makini ili yasileta shida.

Mpendwa ngozi yenye afya haitakiwi kuwa na mafuta wala kuwa kavu...(Oil or Dry skin). Inatakiwa kuwa nyevunyevu (moisturized). Kama sio hivyo tuwasiliane mapema kwa ushauri zaidi.
 
NAMNA YA KUTUNZA NGOZI
.
Hatua ya kwanza ni kusafisha kwa cleanser(sabuni maalumu ya uso tu)
Faida zake
-Inapunguza mafuta,
-Inaondoa vumbi,jasho,moshi, na nakufungua matundu ya ngozi.
Hatua ya pili ni kupaka Tonner
Faida ya Tonner,
-Inaziba matundu yaliyofunguliwa na cleanser,
-Huandaa ngozi kwa ajiri ya mafuta(cream).

Hatua ya tatu ni kupaka cream ya macho. (eye cream).
Faida zake;
-Huondoa mikunjo (makunyanzi kwenye jicho)
-Huo ndoa weusi kwenye jicho.
Hatua ya mwisho ni kupaka cream. Day cream kwa mchana au Night cream kwa usiku.



Hizi ni baadhi ya bidhaa za usoni (skin care produsts) kutoka kampuni yetu ya Oriflame, Karibu sana.

2 comments:

  1. Karibu sana kwa lolote au ushauri comment yako ni mhimu sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari,izo oriflame ni kwa ngozi aina zote?

      Delete